Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazoezi ya viungo yanasaidia kuzuaia saratani huo:WHO

Mazoezi ya viungo yanasaidia kuzuaia saratani huo:WHO

Leo ni siku ya kimataifa ya saratani na kwa mujibu wa shirika la afya duniani Who siku hii ni ya kuelimisha umma kuhusu ugonjwa wa saratani, jinsi ya kuzuai, kuwachagiza kupimwa na kupata tiba.

Siku hii ambayo huadhimishwa kila mwaka February nne inaongozwa na muungano wa kimataifa dhidi ya saratani ambao una jumuisha mashirika zaidi ya 350 ya kupambana na saratani katika nchi zaidi ya 100 duniani.

WHO inasema siku hii inailenga jamii kupitia mawasiliano na kuwashawishi watunga sera kutoa kipaumbele katika kukabiliana na saratani.Kama anavyofafanua Dr. Tim Armstrong,mratibu wa WHO mazoezi ya viungo uanaweza kusaidia kupunguza saratani.

(SAUTI YA TIM AMSTRONG)

Nalo shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA linakadiria kwamba ifikapo mwaka 2030 zaidi ya watu milioni 13 ulimwenguni watakufa na saratani kila mwaka na vifo takribani milioni tisa vitakuwa katika nchi zinazoendelea ingawa nchi zilizoendelea ndizo zenye tatizo kubwa la saratani.