Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mechi ya soka yakusanya nusu milioni za msaada:UM

Mechi ya soka yakusanya nusu milioni za msaada:UM

Mechi ya mchezo wa soka iliyoaandaliwa na Umoja wa Mataifa ikiwakutanisha wachezaji nyota duniani hapo disemba mwaka jana, imefanikiwa kukusanya kiasi cha dola za kimarekani nusu milioni moja .

Mechi hiyo ambayo iliandaliwa kwa ajili ya kuchangisha fedha ili kusizaidia nchi zilizokumbwa na majanga ncHaiti, Pakistan na makundi ya watu walioko pembezoni huko Ugiriki, ilifanyika chini ya uratibu wa shirika la maendeleo la umoja wa mataifa UNDP.

Zaidi ya mashabiki 33,000 walifurika kwenye uwanja wa Karaiskakis, ulioko nje kidogo ya jiji la Athens kushuhudia mechi hiyo. Mkuu wa shughuli za utawala wa UNDP Helen Clark amesema kuwa ametiwa moyo na kuvutiwa kutokana na mafanikio hayo yaliyopatikana kupitia mchezo huo wa soka.