Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchunguzi wa ghasia nchini Misri ufanyike:Pillay

Uchunguzi wa ghasia nchini Misri ufanyike:Pillay

Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kufanyika uchunguzi ulio wazi kuhusu ghasia zilizoshuhudiwa kwenye mitaa ya mji wa Cairo nchini Misri siku ya Jumatano.

Mkuu wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Navi Pillay anasema kuwa waliopanga ghasia hizo ni lazima wajulikane. Pillay pia ameshutumu hatua za kuwakamata na kuwadhulumu waandishi wa habari na watetesi wa haki za binadamu akisema kuwa hilo lilikuwa jaribio la kutaka kuzima kujulikana kilichokuwa kikiendeleda nchini Misri.

Pillay ametoa wito wa kuachiliwa mara moja kwa zaidi ya watetesi 20 wa haki za binadamu waliokamatwa na kufungwa siku ya Alhamisi .

(SAUTI YA NAVI PILLAY)

Pillay ameongeza kuwa ataunga mkono kuitishwa kwa mkutano na baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kujadili hali nchini Misri.