Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miezi sita baada ya mafuriko Pakistan bado ni changamoto:OCHA

Miezi sita baada ya mafuriko Pakistan bado ni changamoto:OCHA

Miezi sita baada ya mafuriko nchini Pakistan mahitaji ya dharura hayaonekani kuisha leo wala kesho huku mamilioni bado wanahitaji msaada kwa mujibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA inakadiria kwamba watu milioni nne bado hawana nyumba za kuishi, na uharibifu wa mazao umewaacha watu milioni 5.5 wakitegemea chakula cha msaada. Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema bado linatoa msaada wa maji safi kwa watu zaidi ya milioni 3.5 Pascal Villeneuve ni kaimu mwakilishi wa wa UNICEF Pakistan.

(SAUTI YA PASCAL VILLENEUVE)

Zaidi ya watu milioni 18 waliathirika na mafuriko nchini Pakistan mafuriko ambayo yamesambaratisha nyumba zaidi ya milioni 1.7 na ekari zaidi ya milioni 2.2 za mazao.