Ban amewataka viongoziAfrika Kaskazini kuzuia machafuko zaidi

28 Januari 2011

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewataka viongozi wa Misri, Tunisia na Yemen kuzuai kuendelea kwa machafuko zaidi.

Akizungumza mjini Davos Ban amesema viongozi wachukulie maandamano yanayoendelea kama fursa ya kuchukua hatua kushughulikia matatizo na matakwa ya watu wao. Katibu Mkuu amesema uhuru wa watu wa kujieleza na kukusanyika lazima uheshimiwe.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Maandamano ya ghasia yamezuka Tunisia, Misri na Yemen wakati watu walipomiminika mitaani kudai uhuru zaidi, ajira na kukomeshwa kwa ufisadi.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud