UNHCR imetoa wito wa kuwalinda wapenzi wa jinsia moja
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema kwamba watu ambao wanabaguliwa kutokana na jinsia au kuwa na wapenzi wa jinsia moja ni lazima wapewe ulinzi wa kimataifa.
Kwa mujibu wa shirika hilo makundi haya yanakabiliwa na hatari na hivyo yasisahaulike. Limeongeza kuwa wakati nchi nyingi zina sheria za kuchukulia kuwa ni hatia mapenzi ya jinsia moja kiwepo kukabiliwa na hukumu ya kifo katika nchi saba hali hii inasababisha matatizo makubwa hususani kwa wakimbizi na waomba hifadhi ambao ni wapenzi wa jinsia moja. Andrej Mahecic ni msemaji wa UNHCR.
(SAUTI YA ANDREJ MAHECIC)
Kali hii imekuja siku chache baada ya mauaji ya mwanaharakati wa haki za wapenzi wa jinsia moja na mpigania haki za binadamu nchini Uganda David Kato. Mauaji yake yamelaaniwa na watu wambalimbali akiwemo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na ukimwi UNAIDS Michel Sidibe ambaye ameitaka serikali ya Uganda kufanya uchunguzi wa kina wa kifo chake na kuhakikisha usalama wa kutosha kwa watu wake ambao ni wasagaji, mashoga, na waliobadili jinsia.