Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutopatikana suluhu Ivory Coast kunatia hofu: Ban

Kutopatikana suluhu Ivory Coast kunatia hofu: Ban

Kukosekana kwa muafaka miongoni mwa viongozi wa Afrika wa jinsi ya kutatua mzozo wa kisiasa nchini Ivory Coast kunatia mhofu amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

Ban amesema atakutana na viongozi wa muungano wa Afrika mjini Addis Ababa Ethiopia kutafuta njia ya amani ya kumaliza mzozo huo. Ivory Coast imekuwa katika mtafaruku wa kisiasa tangu uchaguzi wa Urais wa Novemba 29 mwaka jana .Jumuiya ya kimataifa inaamini Alassane Ouatarra alishinda lakini Rais Laurent Gbagbo amegoma kukabidhi madaraka.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Machfuko hayo ya kisiasa yamewafungisha virago watu zaidi ya 31,000 na kuwa wakimbizi Liberia limesema shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR, huku watu wengine 20,000 wakiwa wakimbizi wa ndani.