Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Amani, usalama na maendeleo vinategemeana:Ban

Amani, usalama na maendeleo vinategemeana:Ban

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linajikita kwa kile linachokiita uhusiano muhimu uliopo baina ya amani, usalama na maendeleo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema nchi 9 kati ya 10 zenye vyanzo hafifu vya maendeleo zimekumbwa na vita katika miaka 20 iliyopita.

Amesema kizazi kijacho chenye changamoto za usalama kitahitaji mbinu za kuzuia migogoro, mikakati ya kupunguza hatari ya majanga,juhudi imara za jamii katika operesheni za amani na kuboresha utawala wa sheria.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Matukio ya hivi karibuni duniani kote ni kumbusho la haja ya kuwa na mifumo imara ya kisiasa ili kusaidia katika amani, fursa, hali bora ya maisha na kuridhika kwa watawaliwa.