Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN-HABITAT na UNEP kusaidia kuboresha usafiri Afrika Mashariki

UN-HABITAT na UNEP kusaidia kuboresha usafiri Afrika Mashariki

Kutokana na mikutano iliyofanyika Nairobi, Kampala na Addis Ababa mapema mwezi huu, shirika la Umoja wa Mataifa la makazi UN-HABITAT na lile la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP wamezindua mpango mpya wa kikanda kuchagiza utekelezaji wa suluhu muafaka za suala la usafiri katika miji ya Afrika Mashariki.

Mradi huo utatekelezwa na UN-HABITAT na utazisaidia serikali za taifa na mikoa katika miji mkikuu ya Ethiopia, Kenya na Uganda katika kutatua matatizo ya usafiri. Jason Nyakundi na ripoti kamili.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)