Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Comoro yapongezwa na UM kwa uchaguzi wa amani wa Rais

Comoro yapongezwa na UM kwa uchaguzi wa amani wa Rais

Watu wa kisiwa cha Comoro wamepongezwa na Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kwa kufanya uchaguzi wa Rais na majimbo.

Matokeo rasmi ya uchaguzi huo uliofanyika Novemba na Desemba mwaka jana yalitolewa Januari 13 mwaka huu. Katika taarifa yake Ban amekaribisha kitendo cha wagombea wote kukubali matokeo ya uchaguzi wa Urais katika muungano wa visiwa vitatu vinavyoonda Comoro katika pwani ya Msumbiji kwenye bahari ya Hindi.

Amepongeza jukumu kubwa lililotokelezwa na muungano wa Afrika kwa kuchagiza kufanyika kwa uchaguzi wa amani na kidemokrasia nchini Comoro.