Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchumi wa nchi zinazoendelea unatia matumaini:Bank ya dunia

Uchumi wa nchi zinazoendelea unatia matumaini:Bank ya dunia

Bank ya dunia imesema uchumi wa dunia hivi sasa unaondoka katika hatua ya kuinuka tena baada ya mdororo ingawa kidogo, lakini unakuwa mwaka huu na ujao huku nchi zinazoendelea zikichangia karibu nusu ya ukuaji wa kimataifa.

Taarifa ya matarajio ya uchumi ya Bank ya dunia kwa mwaka 2011 yanakadiria kwamba pato la taifa la dunia kwa mwaka 2010 liliongezeka kwa asilimia 3.9 na mwaka huu litashuka kidogo hadi asilimia 3.3 kabla ya kukua tena hadi asilimia 3.6 mwaka 2012.

Uchumi wa nchi zinazoendelea unatarajiwa kukua kwa asilimia 6 mwaka huu na asilimia 6.1 mwaka 2012, na utaendelea kuzitangulia nchi zilizoendelea ambazo uchumi wake unatarajiwa kukua kwa asilimi 2.4 kwa mwaka 2011 na 2.7 kwa mwaka 2012. Kama anavyofafanua Andrew Burns meneja wa maendeleo ya kimataifa ya uchumi katika Bank ya dunia.

(SAUTI YA ANDREW BURNS)