Mpango wa UM nchini Sudan unaongeza kasi kwa ajili ya kura muhimu ya maoni mwishoni mwa wiki hii

4 Januari 2011

Rais wa Sudan Omar al-Bashir, yupo ziarani katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba kabla ya kura ya maoni itakayoshuhudia eneo hilo kujitenga ama la hapo Jumapili ijayo.

Kura ya maoni SudanBwana Bashir amekutana na Rais wa eneo linalojitawala la Sudan Kusini , Salva Kiir, kujadili maswala mbali, iwapo raia wa Sudan Kusini wataamua kujitenga na Kaskazini.

Miongoni mwa masuala hayo ni pamoja na usimamizi wa raslimali za maji, mafuta na mustakabal wa raia wa kusini wanaoishi kaskazini.

Rais Omar al-Bashir amesema atasikitishwa sana kuona Sudan itagawanyika na kuwa nchi mbili.Hata hivyo Bw Bashir amesema atafurahi iwapo kuundwa kwa nchi hizo mbili na kuwa mataifa mawili, kutaleta kile alichokiita, amani ya kweli kwa pande zote mbili za Sudan. Kura ya maoni itaanza kupigwa tarehe 9 hadi 15 mwezi huu. Kura hiyo inasimamiwa kwa kiasi kikubwa na Umoja wa Mataifa na Dennis Kadima ni mkuu wa kitengo cha Umoja wa Mataifa cha uchaguzi na kura ya maoni anasema wanatuamai licha ya changamoto kura itaenda salama.

(SAUTI YA DENNIS KADIMA)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter