Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa haki za binadamu auasa utawala wa Ivory Coast

Mkuu wa haki za binadamu auasa utawala wa Ivory Coast

Juhudi za Kidiplomasia za viongozi wa nne wa Afrika zimeshindwa kutatua mvutano wa kisiasa nchini Ivory Coast ambapo Rais Laurent Gbagbo amegoma kuachia ngazi na kumpisha mpinzani wake Alassane Ouattara ambaye ametangaza kuwa muda wa upatanishi na majadiliano umekwisha.

Rais wa Benin, Sierra Leone na Cape Verde wakiwasilisha ECOWAS walikuwa na mazungumzo na pande zote siku ya Jumatatu wakimshirikisha mwakilishi wa muungano wa Afrika waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga lakini mazungumzo hayo hayakuzaa matunda.

Leo kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay amewaandikia mmoja mmoja kundi la viongozi wa ngazi za juu nchini Ivory Coast akiwakumbusha kwamba watalaumiwa na watawajibika kwa ukiakaji wa haki za binadamu kutokana na matendo yao au kuhusika kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

Amesema mfumo wa kimataifa wa uhalifu ulioanzishwa miaka zaidi ya 15 unatoa nyezo ambayo haikuwepo awali ya kuwajibisha wanaohusika na uhalifu. Na hivyo hakuna wakuu wa nchi na wadau wengine ambao watajihakikisha kutekeleza uhalifu na wasiwajibishwe. Lin Sambili na taarifa kamili.

(SAUTI YA LIN SAMBILI)