Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF inasaidia kupambana na Ukimwi DR Congo

UNICEF inasaidia kupambana na Ukimwi DR Congo

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumiwa watoto UNICEF nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limekuwa likianisha kazi za ofisi yake katika mji wa Lubumbashi ambayo ni kupambana ukosefu wa uelewa wa kutosha miongoni mwa watu wa kuzuia virusi vya HIV na ukimwi.

Kwa mujibu wa shirika hilo watu huenda hospitali tuu pale wanapokuwa wagonjwa na hivyo maambukizi ya HIV yanakuwa vigumu kubainika hadi pale mgonjwa anapofikia hali mahtuti na kulazwa hospitali.

Ili kuzuia maambukizi ya virusi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto shirika la afya duniani WHO linashauri kutumia dawa za kufubaza virusi yaani ARV's wakati wa ujauzito na mamia ya wanawake wa Congo wanajifungua kila siku bila kuhudhuria kliniki au kujua kama wanavirusi.

Dr Joe Kabongo naibu mratibu wa UNICEF mjini Lubumbashi anasema ili kuzuia hali hiyo njia za kuzuia maambukizi ya HIV lazima zitumike kwenye vituo vyote vya afya kuanzia ngazi ya chini kabisa kwenye vijiji, na hasa kuwashawishi wanaume ambao katika nchi ya Congo bado ndio wanaofanya maamuzi kuhusu masuala ya kupima na kujua afya zao.