Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP kupunguza tatizo la chakula kwa kununua ngano Afghanistan

WFP kupunguza tatizo la chakula kwa kununua ngano Afghanistan

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP leo limesema litaweza kusaidia tatizo la upungufu wa ngano nchini Afghanistan kwa kununua ngano hiyo kwa kiwango kibubwa nchini humo.

Katika makubaliano maalumu WFP itanunua tani 13,000 za ngano ambazo zinatosha kulisha watu zaidi ya laki tano kwa miezi mitatu, na litanunua ngano hiyo kutoka wizara ya kilimo , umwagiliaji na mifugo ya nchi hiyo.

Fedha za kununulia ngano hiyo ni za msaada kutoka shirika la kimataifa la Marekani la msaada kwa maendeleo USAID. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)