Skip to main content

Ujerumani kusaidia katika usalama wa chakula na kilimo: FAO

Ujerumani kusaidia katika usalama wa chakula na kilimo: FAO

Serikali ya Ujerumani imetoa dola milioni sita kwa ajili ya usalama wa chakula na lishe, maisha endelevu na kilimo bora kinachozingatia hali ya hewa.

Katika fedha hizo zaidi ya doloa milioni mbili zitatumika kufadhili mradi wa miaka mitatu kutathimini na kuweka taarifa za mafanikio ya mpango huo wa msaada wa kuwalisha watu ili kuwaaarifu watunga sera na mipango ya lishe katika nchi zinazoendelea. Miradi mingine miwili inaandaliwa yenye lengo la kuimarisha lishe na elimu ya lishe.