Skip to main content

Wafugaji Turkana Kenya walazimika kuwa wavuvi:IOM

Wafugaji Turkana Kenya walazimika kuwa wavuvi:IOM

Wafugaji wa muda mrefu wanaoshi katika pwani ya ziwa Turkana nchini Kenya wanabadilika na kuwa wavuvi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa kuwalazimu kubadili mfumo wa maisha .

Hayo yamesemwa na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM ambalo limeongeza kuwa kukosekana kwa malisho na ukame unaojirudia katika eneo hilo inamaanisha kwamba jamii za Waturkana hawawezi tena kutegemea ng'ombe, mbuzi na ngamia kuendesha maisha yao.

Kwa mujibu wa msemaji wa IOM Jared Bloch familia 450 zitagawiwa boti za kuvulia na mafunzo ili kuziwezesha kuvua samaki katika ziwa Turkana. IOM itafanikisha kufanya hivyo kwa msaada mkubwa wa serikali ya Japan.