Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban awataka vijana kuunga mkono UM kufikia malengo ya wengi

Ban awataka vijana kuunga mkono UM kufikia malengo ya wengi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewataka vijana kuunga mkono harakati za Umoja huo wa Mataifa, kuhakikisha dunia inaendelea kuwa salama na kimbilio la wengi, pamoja na kwamba changamoto zinazoendelea kuibuka nyakati hizo ni kubwa zisizowahi kushuhudiwa wakati wowote.

Katika hotuba yake aliyoitoa kwenye chuo cha masuala ya Diplomasia na uhusiano wa Kimataifa Ban amesema kuwa ulimwengu unapitia kwenye wakati mgumu kwani watu ake wamekuwa kukumbana na majaribu ya aina mbalimbali, hatua ambayo imefanya kutoweka kwa hali ya kuaminiana na taasisi za kazi na viongozi wake.

Amesema kwa hali kama hiyo, hakuna njia nyingine ya mkato mbali ya kuwa na sura ya mashirikiano na maelewano kwani kinyume cha hapo hali ya baadaye ya dunia itakuwa kwenye hali tete zaidi.

Ban Ki-moon ambaye pia alitunikiwa shahada ya heshima alizungumzia pia changamoto zinazoikabili jumuiya ya Umoja wa Mataifa na akasema kwamba Umoja huo kwa hivi sasa unajikuta ukiwajibika kufanya kazi katika majukumu makubwa zaidi ili kukidhi matarajio ya wengi