Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mipango miji salama kwa wanawake yazinduliwa Delhi

Mipango miji salama kwa wanawake yazinduliwa Delhi

Shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya akina mama limezindua mpango wa kimataifa wa kuifanya miji kuwa salama kwa wanawake mjini New Delhi nchini India wakati wa kuanza kwa mkutano wa kimataifa kuhusu usalama wa wanawake.

Kwa sasa watu bilioni 3.4 wanaishi kwenye maeneo ya miji kote duniani. Visa vya uhalifu katika maeneo haya ni vingi lakini mipango ya maendeleo ya miji mara nyingi inasahau hatari inatowakabili wanawake.

Mpango huo utaangazia zaidi maeneo ya mabanda na miongoni mwa wakaazi maskini wa mijini kwenye miji ya Quito nchini Ecuador , Cairo nchini Misri, New Delhi nchini India , Port Moresby nchini Papua New Guinea na Kigali nchini Rwanda. Kila mji utachangia katika kutafuta njia za kumaliza dhuluma dhidi ya wanawake ambazo zitatumiwa na miji mingine kote duniani.