Skip to main content

IOM yaunga mkono matembezi ya kupinga dhuluma za kijinsia

IOM yaunga mkono matembezi ya kupinga dhuluma za kijinsia

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kwa ushirikiano na wizara ya masuala ya uchumi na jamii nchini Equador litatoa mchango kwa serikali za mitaa mashirika ya kitaifa na kimataifa na yasiyokuwa ya umma kwenye matambezi juma hili ya kupinga dhuluma za jinsia.

Zaidi ya watu 600 watashiriki matembezi hayo yatakayoandaliwa tarehe 25 mwezi huu ili kutoa hamasisho kuhusu tatizo hilo na kuunga mkono njia za kukabiliana nalo.

Tangu mwaka 2008 IOM limekuwa likiendesha kampeni kubwa ya kupinga dhuluma za jinsia katika maoneo ya Limones na San Lorenzo kama mipango ya dharura. Maeneo ya San Lorenzo na Limones yanayopakana na Colombia yanatajwa kama maeneo yaliyo na visa vingi vya dhuluma za jinsia nchini Equador.