Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wawekezaji waonya kutokea kwa hali mbaya ya kiuchumi iwapo hatua hazitachukuliwa

Wawekezaji waonya kutokea kwa hali mbaya ya kiuchumi iwapo hatua hazitachukuliwa

Ulimwengu unakabiliwa na hatari ya hali ngumu ya kiuchumi kuliko iliyoikumba hivi majuzi iwapo serikali , watunzi wa sera na wajumbe kwenye mkutano wa umoja wa mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa hawatachukua hatua za kupunguza mabadiliko ya hali hewa.

Hii ni baada ya wawekezaji kutoka Asia , Afrika , Australia ,Ulaya , Amerika kusini na Marekani ambao wana uwekezaji wenye thamani ya dola trilioni bilioni moja kwa pamoja kuonya kuwa mapato ya kitaifa yanayohusiana kwa njia moja au nyingine na hali ya hewa huenda yakapungua kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2050 kutokana a na mabadiliko ya hali ya hewa. Hili linajiri kabla ya mkutano kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa unaotarajiwa kuandaliwa mjini Cancun Mexico kuanzia tarehe 29 mwezi huu ambapo ulimwengu utajaribu kuafikia makubaliano yatakayochukua mahala pa yale ya Kyoto ambzpo nchi zilizo na utajiri wa kiviwanda ziliafikia makubaliano ya kupunguza gesi inayochafua mazingira.