Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afya duni yachangia kuongezeka kwa umaskini duniani

Afya duni yachangia kuongezeka kwa umaskini duniani

Kulingana na ripoti mpya ya shirika la afya duniani WHO na shirika la makaazi la Umoja wa Mataifa UN HABITAT inaonyesha vile afya duni inachangia kuongezeka kwa viwango vya umaskini mijini.

Ripoti hiyo ina lengo la kuwawezesha viongozi wa miji na wanaotoa mipangilio kwenye miji kutambua waathirika na njia za kuimarisha afya zao. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

Ripoti hiyo ambayo imezingatia utafiti mpya uliobainisha mwenendo wa majiji namna yanavyosahau kutupia jicho baadhi ya maeneo na hivyo kurudisha nyuma maenendeleo ya sehemu mbalimbali.

Hata hivyo ripoti hiyo safari hii pamoja na kuainisha namna takwimu zinavyotofautiana kutoka mji mmoja mpaka mwingine,lakini pia takwimu hizo zinatoa fursa kwa viongozi wa majiji pamoja na watunga sera kufuatulia mwenendo ndani ya miji yao mpaka kwenye maeneo ya jirani ili hatimaye kutoa suluhisho la haraka.

Akizungumzia ripoti hiyo Mkurugenzi Mkuu wa shirika la afya Duniani WHO Dr Dr Margaret Chan amesema kuwa kumekuwa na hali duni ya kiafya na mpangilio wa maisha hasa katika maeneo ambayo yanajulikana kama maeneo ya vichochoroni kwani hali halisi inaonyesha kuwepo kwa tofauti kubwa kwa wakazi hao wa maeneo ya mijini ambao hutufautiana katika kufikiwa na huduma za kiafya

Ripoti hiyo imetahadharisha kuwa kama hakutachukuliwa juhudi za haraka kubadili mfumo huo nchi nyingi zinakabiliwa na hali ya shaka shaka ya kufikia malengo ya maendeleo ya milenia.