Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sauti ya wanyinge lazima isikike kwenye G-20:Ban

Sauti ya wanyinge lazima isikike kwenye G-20:Ban

Mkutano mataifa 20 yanayoongoza kiuchumi duniani G-20 karibu unaanza mjini Seoul Korea ya Kusini.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini humo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema mkutano huo unaoanza kesho ni lazima uzingatia mahitaji ya wasiojiweza.

Ban amabaye atahudhuria mkutano huo pia ameongeza kuwa dunia haiwezi kuendelea endapo asilimia kubwa ya watu bado ni masikini amesema watu milioni 64 wamelazimika kuingia kwenye umasikini uliokithiri mwaka huu pekee.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Ameongeza kuwa huu ni wakati wa mshikamano huku akisisitiza masuala matatu muhimu uwekezaji, mabadiliko ya ahali ya hewa na malengo ya maendeleo ya milenia aliyosema ni ya ujenzi wa amani, kuleta matumaini na kuwa na dunia bora kwa wote, na ndio maana anayaata malengo hayo silaha za ujenzi.