Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ECOSOC yachaguwa wakurugenzi 41 wa bodi ya chombo cha UM cha wanawake UN-Women

ECOSOC yachaguwa wakurugenzi 41 wa bodi ya chombo cha UM cha wanawake UN-Women

Baraza la kiuchumi na kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC leo limekutana kuchagua bodi ya wakurugenzi wa chombo kipya cha Umoja wa Mataifa kinachoshughulikia masuala ya usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake UN-Women.

Uchaguzi huo unafanyika kwa kuzingatia azimio la baraza kuu la Umoja wa Mataifa la Julai pili mwaka huu, na azimio la baraza la usalama la septemba na Oktoba mwaka huu. Akizungumza wakati wa kuanza zoezi hilo la upigaji kura rais wa ECOSOC Hamidoun Ali amesema wajumbe 41 watachaguliwa

(SAUTI YA HAMIDOUN ALI)

Mbali ya uchaguzi huo baraza la ECOSOC pia litapendekeza mada ya kujadiliwa na mswada wa maamuzi ya mkutano wa ngazi ya juu wa baraza hilo unaotarajiwa kufanyika mwaka 2011.