Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ILO yaarifu kuanza kutengamaa kwa ajira

ILO yaarifu kuanza kutengamaa kwa ajira

Takwimu mpya zilizotolewa leo na shirika la kazi duniani ILO zinaonyesha kuwa tatizo la ajira duniani limeanza kutengamaa huku kukiwa na tofauti katika sekta za uchumi na kuimarika kwa nafasi za kazi katika nusu ya mwaka huu.

Takwimu hizo ni za matokeo ya utafiti yaliyokusanywa katika sekta 13 kutoka nchi 51 zilizoendelea na zinazoendele. Na matokeo hayo yameonsha kutokuwepo kwa uwiano, kwani wakati sekta ya ujenzi na viwanda ikiwa imepoteza nafasi za kazi milioni tano katika robo ya kwanza ya mwaka huu sekta ya afya imeongeza karibu nafasi milioni 2.8 za kazi.

Kwa mujibu wa ILO mwaka huu wa 2010 uchumi wa dunia umeingia katika hatua mpya ambapo tofauti na uwiano katika masoko ya kazi vimeongezeka, huku hali ya uchumi ikisalia kuwa tete katika baadhi ya nchi na sekta za fedha haziaimarika.