Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Biashara na uchumi ni muhimu kwa malengo ya milenia:Ban

Biashara na uchumi ni muhimu kwa malengo ya milenia:Ban

Wakati ulimwengu unapojikakamua kujikwamua kutoka kwa hali mbaya ya kiuchumi katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea umuhimu wa sekta za kibiashara na kifedha katika kushughulikia masuala yakiwemo ya kimaendeleo na mabadiliko ya hali ya hewa.

Kwenye ujumbe uliosomwa kwa niaba yake mjini Beijing China na mratibu wa Umoja wa Mataifa Renata Lok Dessallien wakati wa mkutano kimataifa wa kichumi mwaka 2010 Ban alisema kuwa kujenga ulimwengu ulio na maendeleo ni muhimu kwa uchumi.

Ban amesema kuwa katika majuma yajayo mataifa ya G20 yataandaa mkutano mjini Seoul nchini Korea kusini ambapo suala la maendeleo litakuwa ajenda kuu kabla ya mkutano wa Cancun Mexico utakaojadili mabadiliko ya hali ya hewa mkutano ambao anasema utakuwa mtihani kwa nchi zilizostawi.

Ban pia amesema kuwa miaka miwili kutoka sasa nchi zitarejea mjini Rio de Janeiro nchini Brazil kutia nguvu makubalino ya kimaendeleo yenye nguzo tatu yakiwemo maendeeleo ya kiuchumi ya kijamii na utunzi wa mazingira yaliyoafikwa mwaka 1992 kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa.