Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amewashauri vijana kutumia sauti na uwezo wao kuleta maelewano

Ban amewashauri vijana kutumia sauti na uwezo wao kuleta maelewano

Katibu mkuu wa umoja wa umoja Ban ki Moon amewashauri vijana kutumia uwezo walio nao kwa manufaa ya kuleta uelewano katika ulimwengi wa sasa ambao unashirikiana katika masuala mengi.

Akihutubia mkutano wa vijana unaondaliwa mjini kuala Lumpur nchini Malaysia kwa njia ya video Ban amewashauri vijana hao ana kusema kuwa maamuzi pamoja na vitendo vyao huwa vinachangia mabadiliko na kuwa wao ndio viongozi wa kesho .

Zaidi ya awanafuzi 1000 kati ya miaka kumi na nane na ishirini na minne wanahudhuria mkutano huo wenye kauli mbiu kuunganisha tamamduni kwa amani na maenedeleo. Kwa muda wa siku tano za mkutano huo wanafunzi kutoka kila sehemu ya dunia watashiriki vikao sawia na wanadiplomasia wa kigeni kulingana na mpangilo wa umoja wa mataifa.