Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wataka mapinduzi kwenye teknolojia ya simu na mtandao

UM wataka mapinduzi kwenye teknolojia ya simu na mtandao

Shirika la Umoja wa Mataita linalohusika na masuala ya mawasiliano, limezitaka mamlaka kuhakikusha kwamba zinafanyia mapinduzi mifumo ya mawasiliano kama vile kupanua uwigo wa mitandao ya simu za mikononi duniani kote, na kisha kufanya jambo kama hilo hilo kwa internet.

Akizungumza kwenye kongamano la kimataifa linalofanyika Dakar, Senegal Katibu Mkuu wa shirika la kimataifa la mawasiliano ITU, Hamadoun Touré ametaka mifumo hiyo kuingizwa kwenye mitandao inayofanya kazi kwa mfumo wa broadband ambayo huenda mbali zaidi na kwa kasi ya hali ya juu

Bwana Touré,amesema kuwa mitando ya simu na internet inahitajika kubadilika sasa na kuingizwa kwenye maajabu mapya ya matumizi ya broadband. Hata hivyo ametaka mamlaka kuanza kuweka kipaumbele kusambaza mifumo inayotumia teknolojia ya broadband ili iwe rahisi zaidi kupatikana na kuanza kutumiwa