UM kuendelea kuisaidia Sudan kufanikisha kura ya maoni

2 Novemba 2010

Umoja wa Mataifa umesema kuwa uko tayari kutoa msaada wa hali na mali ili kufanikisha zoezi la upigaji w akura ya maoni nchini Sudan juu ya ama Sudan kusin ijitenge ama au la.

Ikiwa imesalia wiki mbili ili kuanza kwa zoezi la uandikishwaji kwenye daftari la wapiga kura, Mkurugenzi wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia zoezi hilo la kura ya mano UNIRED Denis Kadima amesema kuwa Umoja huo wa Mataifa unatazamia kuanza kusafirisha vifaa vya kujiandishia kwenye daftari hilo hadi mji mkuu wa Juba.

UNIRED inatazamia pia kupeleka wataalamu wake kwenye eneo hilo kwa ajili ya kutoa mafunzo waandikishaji 11,000 wataotawanywa kwenye vituo mbalimbali. Ama umoja huo wa Mataifa upo mbioni kutoa misaada mingine mbalimbali ikiwemo ile kiufundi kwa shabaya hiyo hiyo ya kufanikisha zoezi la upigaji kura.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter