Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wataja vipaumbele ili kuleta usawa kwenye elimu

UM wataja vipaumbele ili kuleta usawa kwenye elimu

Jopo la wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa wanaoshughulika na upatikanaji elimu kwa wote. wametaja vipambele ambavyo vinaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kupunguza pengo la kukosekana kwa usawa kwenye utoaji elimu.

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu suala la elimu kwa wote, Kishore Singh amesema ,kuna haja sasa ya kuangalia namna mfumo wa utoaji elimu pamoja na namna ya kuwapata walimu bora ili kufikia shabaya ya kuwa na usawa kwenye elimu.

Hoja nyingine aliyozingatia mtaalamu huyo ni umuhimu wa kufadhilia miradi ya kiubunifu itayoangazia mifumo ya utoaji elimu.  Amesema ili shabaya ya kuwa na usawa kwenye elimu, lazima pia kutambua kuwa kila mhusika anatimiza wajibu wake ikiwemo wazazi, watumishi wa umma, watoa huduma binafsi na wanafunzi wenyewe kwa ujumla.

Hata hivyo amehaidi kuendelea kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazorudisha nyuma usawa wa upataji elimu ikiwemo vitendo vya unyanyasaji ambavyo huwanyima fursa baadhi ya makundi ya watu kupata elimu.