Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Takwimu ni nyenzo muhimu sana kwa huduma za jamii: Ban Ki-moon

Takwimu ni nyenzo muhimu sana kwa huduma za jamii: Ban Ki-moon

Leo ni siku ya kimataifa ya takwimu na Umoja wa Mataifa unasema takwimu ni muhimu sana katika maisha ya sasa.

Katika ujumbe maalumu wa kuadhimisha siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema takwimu ni muhimili wa masuala mbalimbali ya serikali, biashara na maamuzi makuu ya jamii. Ban amesema takwimu zinatoa taarifa na mwelekeo na masuala yanayoathiri maisha ya watu, pia ni nyenzo muhimu katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii, ikiwemo juhudi za kufikia malengo ya maendeleo ya milenia.

Ameongeza kuwa ili maendeleo yaweze kupatikana tunahitaji kukusanya takwimu hasa kwa kuangalia kiwango cha umasikini, upatikanaji wa elimu na maradhi, hivyo takwimu ni kiini cha kuweza kupanga bajeti na masuala yote hayo na zaidi.