Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake wanajukumu kubwa katika amani:UNFPA

Wanawake wanajukumu kubwa katika amani:UNFPA

Ubaguzi dhidi ya wanawake na kutendewa ukatili kama ubakaji vimeelezwa kuwa vikwazo vikubwa vya amani, usalama na maendeleo katika nchi na jamii zilizota kwenye vita.

Haya yamo kwenye ripoti ya 2010 ya mtazamo wa idadi ya watu iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA. Ripoti hiyo inasema wakati ambapo wanawake wanapata haki na fursa sawa kama wanaume wanaweza kuhimili majanga na wanaweza kusaidia haraka ujenzi mpya na juhudi za amani katika jamii.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa sauti ya wanawake lazima isikike katika mikataba ya amani na mipango ya ujenzi mpya kama anavyofafanua Safiye Cagar kutoka UNFPA.

(SAUTI YA SAFIYE CAGAR)

Ripoti hiyo ya 2010 ya mtazamo wa idadi ya watu duniani imetolewa sambamba na maadhimisho ya miaka 10 ya azimio namba 1325 la baraza la usalama lililo na lengo la kukomesha ukatili wa kimapenzi dhidi ya wanawake na wasichana katika maeneo ya vita na kuchagiza ushiriki wa wanawake katika mipango ya amani.