Mamilioni wasio na utaifa wanahitaji msaada:UNHCR
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR leo limetoa wito wa serikali kufanya juhudi za haraka kuwasaidia mamilioni ya watu wasio na utaifa wowote.
Kwa mujibu wa shirika hilo watu takriban milioni 12 hawana utaifa, na limesema wanahitaji msaada kutokana na mikataba milwili ya kimataifa ule wa 1954 unahusiana na watu wasio na utaifa na ule wa 1961 wa kupunguza tatizo la watu wasio na utaifa. Wito huo umetolewa na mkurugenzi wa UNHCR wa masuala ya kuwalinda watu kimataifa Volker Turk.
(SAUTI YA VOLKER TURK)
Bwana Turk ameonya kwamba hatua ya polepole ya kushughulikia tatizo hilo inamaanisha kwamba mamilioni ya watu wameachwa njia panda hasa katika masuala ya kisheria huku wakipoteza haki zao nyingi za binadamu.