Skip to main content

Ban amewataka wakuu wa nchi kutimiza ahadi za malengo ya milenia

Ban amewataka wakuu wa nchi kutimiza ahadi za malengo ya milenia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akifunga mkutano wa tathimini ya malengo ya maendeleo ya milenia mjini New York amesema wanachama wote wa Umoja wa Mataifa lazima watimize ahadi ya kufikia malengo hayo hapo 2015.

Ban pia amewataka wakuu wa nchi na wawakilishi wa serikali zaidi ya 130 waliohudhuria mkutano huo wa siku tatu wa malengo ya milenia kufikiria mipango ya muda mrefu zaidi ya 2015.

(SAUTI YA BAN)

Anasema lazima tuhakikishe kwamba ahadi tulizoweka zinakuwa ni ahadi tunazotimiza kwani athari za kutofanya hivyo ni kubwa ,madeni, maradhi na matatizo itakuwa ni kupoteza fursa kwa mabilioni ya watu. Lazima tuwajibishane, mfumo wa Umoja wa Mataifa na mimi tutafanya kila liwezekanalo kuhakikisha uwajibikaji katika pande zote . Ninawaomba pia nyote kufikiria mipango ya muda mrefu hata wakati mnapoongeza juhudi kufikia malengo katika miaka mitano ijayo