Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa malengo ya maendeleo ya milenia unaelekea ukingoni New York:

Mkutano wa malengo ya maendeleo ya milenia unaelekea ukingoni New York:

Mkutano wa siku tatu wa viongozi wa dunia kuhusu hatua zilizopigwa kufikia malengo ya amaendeleo ya milenia utamalizika leo mjini New York.

Viongozi , wakuu wa nchi na wawakilishi wa serikali 130 watakamilisha kutoa taarifa zao za maendeleo waliyopiga kutimiza malengo hayo manane ifikapo 2015. Ikiwa imesalia miaka mitano tuu kabla ya muda wa mwisho kutimiza malengo hayo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameonya kuwa nchi ambazo hazijaendelea zinazidi kughubikwa na umasikini.

Amesema ingawa kuna mafanikio makubwa katika kupunguza vifo vya watoto wachanga na kuweza kupata maji safi nchi hizo ambazo pia huitwa LCD's zinakabiliana na changamoto kubwa kutimiza malengo yote manane. Ban ametoa wito kwa nchi tajiri kutositisha ahadi za msaada wao kwa nchi masikini na kuokoa maisha ya mamilioni ya watu.