Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa tathmini ya malengo ya milenia wakunja jamvi New York

Mkutano wa tathmini ya malengo ya milenia wakunja jamvi New York

Mkutano wa siku tatu wa tathimini ya hatua zilizopigwa katika kufikia malengo ya maendeleo ya milenia umemalizi jioni ya leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.

Mkutano huo uliokuwa unafanyika katika kikao cha 65 cha baraza kuu la Umoja wa Mataifa umehudhuriwa na wakuu wa nchi na wawakilishi wa serikali 130. Mkutano huo umeumeridhia masuala kadhaa ya kutekeleza kabla ya muda wa mwisho wa kutimiza malengo ya milenia kufika hapo 2015. Na kubwa zaidi ni kutimiza ahadi, kuungana pamoja kufikia malengo hayo.

Mkutano huo wakuu na wawakilishi wa nchi wamesema kwa pamoja tutashirikiana kuimarisha masuala ya kiuchumi na maendeleo kwa kila mtu, wataendelea kuongozwa na nia na taratibu za mkataba wa Umoja wa Mataifa kwa kuzingatia sheria za kimataifa na misingi yake.

Pia wameahidi kuzingatia umuhimu wa uhuru, amani na usalama pia kuheshimu haki za binadamu ikiwa ni pamoja na haki ya maendeleo, utawala wa sheria, usawa wa kijinsia na kuzingatia jamii za kidemokrasia kwa ajili ya maendeleo. Hali kadhalika kuhakikisha umasikini umetokomezwa, elimu imepewa kipaumbele na maradhi kuwa historia ifikapo 2015.

Akizungumza katika kufunga mkutano huo Rais Barak Obama wa Marekani nchi ambayO imeahidi kuongeza msaada ili kuzisaidia nchi masikini kutimiza malengo hayo amesema pamoja na jitihada zilizofikiwa hadi sasa nchi tajiri lazima zinyooshe mkono kuoa zaidi , nchi masikini kujitahidi na jumuiya ya kimataifa kubadili mtazamo kuhakikisha malengo hayo yanafikiwa la sivyo ikiwa imesalia miaka mitano tuu itakuwa vigumu.

(SAUTI YA BARAK OBAMA)

Hata hivyo wakuu hao wan chi na wakilishi mbalimbali wa serikali wataendelea kusalia mjini New York kwa ajili ya mjadala rasmi wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa unaoanza kesho Alhamisi, na miongoni mwa watu watakaohutubia mjadala huo ni Rais Inacio Lula da Silva wa Brazili, Rais Barak Obama wa Marekani, Rais Mwai Kibaki wa Kenya, Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran na wengine wengi.