Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tofauti za kijinsia zitokomezwe kufikia malengo ya milenia:Migiro

Tofauti za kijinsia zitokomezwe kufikia malengo ya milenia:Migiro

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose Migiro ametoa wito kwa washiriki wa kongamano la kimataifa la masuala ya jinsia na malengo ya maendeleo mjini Athens Ugiriki, kuchukua hatua haraka kukshughulikia tofauti za kijinsia ambacho ndio chanzo cha ngamamoto zilizopo za maendeleo.

Bi Migiro amesema mara nyingi serikali zimeshindwa kutumia fursa ya matokeo ya kuwawezesha wanawake. Migiro ameliambia kongamano hilo litakaloendelea kwa siku tatu kwamba hii ndio sababu ya pengo la kijinsia katika masuala ya umasikini, elimu, afya na haki za binadamu bado lipo na katika baadhi ya maeneo linaendelea na hata katika nchi tajiri.

Migiro amesema kuna makubaliano katika ngazi ya kitaifa na kimataifa ya kufikia malengo ya maendeleo ya milenia ifikapo mwaka 2015, na amesema ili ndoto hiyo itime lazima serikali zijumuishe katika sera zake masuala ya usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake.