Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Fursa za ajira na usawa ni muhimu katika uchumi:ILO

Fursa za ajira na usawa ni muhimu katika uchumi:ILO

Shirika la kazi duniani ILO limesema ili kukabiliana na matatizo ya kiuchumi yaliyoikumba dunia ni muhimu kuunda nafasi za ajira na kuwa na usawa.

Shirika hilo linasema nafasi mpya zaidi ya milioni 440 za kazi zitaundwa katika nchi zinazoendelea katika kipindi cha miaka 10 ijayo ili kuweza kumudu idadi ya watu wapya wanaoingia katika soko la kazi na kumaliza tatizo la ajira lililochochewa na matatizo ya sasa ya kiuchumi.Taarifa zaidi na Jason Nyakundi.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

"Wito huu umetolewa kupitia kwa ripoti ya ILO pamoja na shirika la fedha duniani IMF kabla ya mkuutano utakaoandaliwa tarehe 13 mwezi huu mjini Oslo kujadili njia za kubuni nafasi za ajira na kuboresha uchumi. Mkutano huo wa siku moja utawaleta pamoja viongozi wa kisiasa na wa kibiashara wakiwemo pia wasomi. Kwa sasa shirika la ILO linakadiria kuwa idadi ya wasiokuwa na ajira imeongezeka kwa zaidi ya watu milioni 30 kote duniani tangu mwaka 2007.

ILO pia linasemakuwa kuwa kwa sasa watu milioni 210 hawana ajira ikiwa ni idadi kubwa zaidi katika historia . Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Geneva jana Jumatano naibu mkurugenzi wa shirika la ILO Philippe Egger amesema kuwa kutokuwepo kwa usawa ndicho chanzo kikuu cha hali iliyo kwa sasa."