Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa shirika la UNAIDS aipongeza Japan kwa kufadhili vita dhidi ya magonjwa ukiwemo ugonjwa wa Ukimwi

Mkuu wa shirika la UNAIDS aipongeza Japan kwa kufadhili vita dhidi ya magonjwa ukiwemo ugonjwa wa Ukimwi

Mkurugenzi wa shirika la misaada la Umoja wa Mataifa UNAIDS Michel Sidibé amempongeza waziri mkuu wa Japan Naoto Kan kwa kujitolea kwa nchi yake kwenye utoaji wa misaada.

Kwa sasa Japan imewekeza zaidi ya dola bilioni moja kusaidia kupambana na ugonjwa wa Ukimwi kwenye nchi maskini tangu mwaka 2002. Japan ndiyo mfadhili mkubwa kwa shughuli ya kupambana na maradhi ya kifua kikuu na malaria iliyobuniwa kwenye mkutano wa nchi tajiri kiviwanda za G8 ulioandaliwa katika kisiwa cha Okinawa nchini Japan mwaka 2000. Akiongoea kwenye warsha moja ya maonyesho ya picha mjini Tokyo,  Kan amezungumzia kujitolea kwa nchi yake kushinikiza kuwepo kwa ufadhili wa vita dhidhi ya ugonjwa wa ukimwi kwenye mkutano unaokuja kuhusu malengo ya milenia. Hii ndio ziara ya kwanza rasmi ya Sidibe nchini Japan ambapo pia aliozindua kampeni ya shirika la UNAIDS yenye kauli mbinu, "yape maradhi ya Ukimwi kadi nyekundu".