Umoja wa Mataifa watafuta njia za kulinda haki za watu walemavu
Watu walio na umelavu wanastahili kupata usaidizi ili kuwawezesha kutekeleza kazi zao. Akiongea kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa wa kutafuta njia za kulinda haki za watu walio na ulemavu mjini New York mwenyekiti wa kamati inayowashughulikia watu walio na ulevamu Ron McCallum amesema kuwa kamati hiyo inahitaji ufadhili utakaoiwezesha kuendeleza majukumu yake.
McCallum ambaye mwenyewe hana uwezo wa kuona pia amesema kuwa ni bahati kubwa kwa kuwa kamati hiyo imepokea bidhaa zitakazowasaidia kutekeleza majukumu yao lakini hata hivyo amesema kuwa wengi wa wanachama wa kamati hiyo hawana vifaa vinavyotumia teknolojia ya kisasa.
Mkutano huo wa siku tatu uliandaliwa ukiwa na kauli mbiu kujumuishwa kwa watu walio na ulemavu kama moja ya njia ya kutekelezwa kwa makubalino ya haki za watu walemavu.