Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNEP akabidhi tuzo lake la Tallberg kwa waathirika wa mafuriko Pakistan

Mkuu wa UNEP akabidhi tuzo lake la Tallberg kwa waathirika wa mafuriko Pakistan

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhifadhi mazingira Achim Steiner, ametoa kiasi cha dola za kimarekani 70,000 ambazo alizipata kupitia tuzo la Tallberg ili kusadia juhudi za uimarishwaji wa hali za kibanadamu nchini Pakistan nchi ambayo iliyokumbwa namafuriko makubwa na waathiri malioni ya watu.

Kufuatia hali mbaya inayoendelea kuwakabili wanachi wa Pakistan ambao wengi wao wameendelea kukosa chakula na makazi, Achim Steiner amesema kuwa atazitoa fedha hizo kwa waathirika hao, na kuhimiza watu wengi kujitolea kwa hali na mali kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa Pakistan.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa tuzo hilo inayofikia thamani ya dola 70, 000 Achim Steiner amesema hali ni mbaya sana nchini Pakistan na hakuna kiti chema kinachoweza kuwafariji raia wa eneo hilo kama kuwajali na kuwafikia na mahitaji yao.

End