Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa UM wahimiza ungaji mkono zaidi kutekelezwa mkataba juu ya kutoweka watu

Wataalamu wa UM wahimiza ungaji mkono zaidi kutekelezwa mkataba juu ya kutoweka watu

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wenye jukumu la kusaidia familia kujua hatima au mahala waliyopo jamaa zao walopotea anahimiza mataifa kueleza kwamba kutoweka kwa nguvu watu ni uhalifu na wasaidiye katika utekelezaji wa mkataba unaokabiliana na tatizo hili.

Katika taarifa kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Kutoweka Watu, leo Jumatatu, tume ya Umoja wa Mataifa juu ya kutekelezwa kutoweka watu kwa nguvu imeyahimiza mataifa ambayo hayakuidhinisha mkataba wa kimataifa juu ya kumlinda kila mtu kutokana na kutoweka kwa nguvu, wafanye hivyo kwa haraka iwezekanavyo. Mkataba huo uloidhinishwa na Baraza Kuu 2006 umetiwa saini na mataifa 83 na kuidhinishwa na mataifa 19 hadi hivi sasa.

Mkataba unaeleza kutoweka kwa nguvu kua ni hatua ya kukamatwa, kuwekwa kizuizini, kutekwa nyara au njia nyengine yeyote ya kunyima uhuru wa mtu na taifa na kufuatia hatua ya kukana kutambua kunyimwa kwa uhuru huo au kuficha mahala mtu amepotelea.