Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ahimiza NGO's kuhamasisha serikali kufikia malengo ya Afya Duniani.

Ban ahimiza NGO's kuhamasisha serikali kufikia malengo ya Afya Duniani.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito kwa mashirika yasiyo ya kiserikali kuongeza juhudi zao ili kuendelea na ahadi ya kuokoa maisha ya wanawake na watoto.

(SAUTI YA KM BAN)

Mkutano huo wa siku tatu unalengo la kuhamasisha uungaji mkono wa kufikiwa malengo kadhaa ya kijami, afya na kiuchumi ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia, MDG's kabla ya mkutano wa viongozi mwezi ujao kutathmini maendeleo ya malengo hayo. Zaidi ya wajumbe 1,400 kutoka mataifa 70 wanahudhuria mkutano huo mkubwa kabisa kuwahi kuandaliwa na Umoja wa Mataifa huko Australia.

Akizungumza kwenye kikao cha ufunguzi pia mkurugenzi mkuu wa Idara ya Ukimwi ya Umoja wa Mataifa Bw. Michele Sidibe aliwaambia wajumbe kwamba wamekua na jukumu muhimu kabisa katika kuhamasisha matatizo ya ugonjwa wa HIV Ukimwi, na kufikisha mipango ya tiba katika maeneo ya mbali kabisa duniani.