Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukizindua mwaka wa kimataifa wa vijana UM umetoa wito wa kuwa na majadiliano na heshma katika vizazi vote

Ukizindua mwaka wa kimataifa wa vijana UM umetoa wito wa kuwa na majadiliano na heshma katika vizazi vote

Mwaka wa kimataifa wa vijana umezinduliwa leo na Umoja wa Mataifa kwa wito wa kukumbatia vipaji, mawazo na nguvu waliyonayo vijana katika kuchagiza utengamano mzuri na majadiliano baina ya vizazi, tamaduni na dini tofauti.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni mazungumzo na utengamano, kauli ambayo imezinduliwa rasmi leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa ikienda sambamba na siku ya kimataifa ya vijana ambayo huadhimishwa kila mwaka 12 Agosti. Katika ujumbe wake maalumu kwa siku hii Katibu Mkuu Ban Ki-moon amezitaka nchi wanachama wa Umoja huo kuongeza uwekezaji katika mipango ya uchumi na jamii ambayo inawafaidi watu takribani milioni 1.2 duniani walio na umri kati ya miaka 15 na 24.

(SAUTI YA BAN  KI-MOON)

Katika kuadhimisha siku hii shirika la kazi dunia ILO limetoa ripoti jana inayoonyesha kwamba tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana limefikia kiwango kikubwa kabisa. Kwa mujibu wa ripoti hiyo kati ya vijana milioni 620 walio na nguvu ya kufanya kazi kote duniani , milioni 81 kati yao hawakuwa na ajira kufikia mwisho wa mwaka jana. ILO imeonya juu ya uwezekano wa kizazi kilichopotea cha vijana kutokuwepo kwenye soko la kazi, na kupoteza matumaini Sara Elder ni mwanauchumi katika shirika la ILO

(SAUTI YA SARA ELDER- ILO)

Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la makazi UN-HABITAT limetangaza kwamba litatoa msaada kwa miradi 51 iliyopendekezwa na vijana katika nchi 31. Fedha hizo zitatoka kwenye mfuko wa mipango maalumu ya vijana mijini ambao hutoa ufadhili wa dola milioni moja kila mwaka.