Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hofu ya chakula imepungua Zimbabwe kwa kuongeza kilimo:UM

Hofu ya chakula imepungua Zimbabwe kwa kuongeza kilimo:UM

Taarifa ya pamoja ya shirika la chakula na kilimo FAO na mpango wa chakula duniani WFP inasema hofu ya upungufu wa chakula imepungua kwa kiasi kikubwa nchini Zimbabwe.

Taarifa hiyo inasema ni kutokana na juhudi kubwa za serikali na msaada wa kimataifa wa dola milioni 70 zilizotumika kuwapa wakulima pembejeo, lakini nchi hiyo bado inahitaji msaada wa kilimo na chakula kwa watu milioni 1.68 kwa mwaka mmoja ujao.

Mpango wa pamoja wa WFP na FAO mwezi Juni mwaka huu ulibaini kuwa kilimo cha mahindi ambacho ni chakula kikuu nchini humo kimeongezeka kwa asilimia 20 mwaka 2010 ikiwa ni kiwango kikubwa kabisa katika kipindi cha miaka 30, na kufanya uzalishaji kuwa juu ikilinganishwa na mwaka 2009. Emilia Casella ni msemaji wa WFP

(SAUTI YA EMILIA CASELLA )