Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baroness Amos ateuliwa kuwa mratibu mpa wa masuala ya kibinadamu wa UM

Baroness Amos ateuliwa kuwa mratibu mpa wa masuala ya kibinadamu wa UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemteua Baroness Amos kuwa mwakilishi wake katika kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura.

Baroness Valarie Amos ambaye ni raia wa Uingereza atachukua nafasi ya John Holmes anayemaliza muda wake. Akizungumzia uteuzi huo waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague amesema, nimefurahi kwa Baroness Amos kuteuliwa kuwa mratibu wa masuala ya kibinadamu na misaada ya Ddharura kumuwakilisha Katibu Mkuu.

Atachangia utaalamu mkubwa alionao, uchapaji kazi na ari katika jukumu lililokuwa likifanywa na John Holmes. Naye waziri wa maendeleo ya kimataifa Andrew Mitchel amese bi Amos katika jukumu lake jipya atakuwa kinara wa haki na mahitaji ya watu atakaowatumikia. Pia amempongeza mratibu anayeondoka John Holmes kwa kazi kubwa aliyoifanya kwa kujiamini, ujuzi na kujitolea kuwasaidia watu.