Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yamtunukia tuzo ya wakimbizi ya Nansen mwandishi mpiga picha

UNHCR yamtunukia tuzo ya wakimbizi ya Nansen mwandishi mpiga picha

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR leo limemtangaza mshindi wa mwaka huu wa tuzo ya wakimbizi iitwayo Nansen Refugee Award kuwa ni mwandishi mpiga picha wa Kiingereza Alixandra Fazzina.

Bi Fazzina amechakuliwa kutokana na kujitolea kwake bila kuchoka kutafuta na kutangaza mambo ambayo mara nyingi yahapewi uzito ambayo ni athari za vita kwa binadamu. Kwa miaka kumi iliyopita Fazzina bila kuchoka ameujulisha ulimwengu athari hizo kwa kutumia picha . Kazi yake imempeleka Fazzina Ulaya, Afrika, Mashariki ya Kati na Asia kuripoti zahma zinazowakumba binadamu ambazo kusahaulika na vyombo vikubwa vya habari.

Baada ya kutangazwa mshindi bi Fazzina amesema "nina furaha isiyo kifani kutambuliwa na UNNHCR na kupewa tuzo hii. Sehemu kubwa ya kazi yangu inabainisha adha za wakimbizi na wakimbizi wa ndani na lengo langu siku zote ni kuelimisha kuhusu waliolazimika kukimbia vita, migogoro na matatizo.

Kuacha nyumba zao na kuhangaika kujenga upya maisha yao ambayo ni changamoto kubwa kukabiliana nayo. Nchi ambazo Fazzina amefanya kazi yake ni pamoja na Bosinia, Kosovo, Somalia, Uganda, Angola, Sierra Leone, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Afghanistan, na Pakistan.