Skip to main content

Mfuko wa jinsia umetoa dola milioni 27.5 kuwawezesha wanawake

Mfuko wa jinsia umetoa dola milioni 27.5 kuwawezesha wanawake

Mfuko wa masuala ya kijinsia umetangaza msaada wa fedha wa milioni 27.5 utakaogawiwa kwa nchi 13 ili kuharakisha mchakato wa kuwawezesha wanawake.

Kila nchi itapata karibu dola milioni 3, na mfuko huo wa masuala ya kijinsia unasaidiwa na michango kutoka kwa serikali za Hispania na Norway, na unasimamiwa na mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo

kwa wanawake UNIFEM ambao ni sehemu ya chombo kipya cha UN women. Msaada huo wa fedha una lengo la kuharakisha hatua za kuchukuliwa katika sera na sheria za kitaifa ili kuimarisha usawa wa kijinsia.

Mwezi Desemba mwaka jana msaada mwingine kama huo ulitolewa kwa nchi 26. Fedha hizo ni sehemu ya dola milioni 68 za miradi na programu mbalimbali zenye nia ya kuchagiza kufikia malengo ya maendeleo ya milenia.