Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ILO Inasisitiza haja ya suluhisho la kimataifa kwa matatizo ya uchumi

ILO Inasisitiza haja ya suluhisho la kimataifa kwa matatizo ya uchumi

Shirika la kazi duniani ILO linasema mdororo wa uchumi ulioikumba dunia na matatizo ya kifedha ni makubwa.

Mkurugenzi msaidizi wa ILO ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa kitengo cha kuilinda jamii katika masuala ya kazi cha ILO Assane Diop amesema kiwango cha ukosefu wa ajira na umasikini kinaongezeka katika kasi ya kutisha.

Akizungumza katika mkutano wa baraza la jamii na uchumi ECOSOC ambalo lilikuwa likijadili masuala ya uchumi, Diop amesema suluhisho la kimataifa linahitajika kwa matatizo haya na nchi zote lazima zitimize wajibu wake ili kufanikiwa kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia.

(SAUTI YA ASSANE DIOP)