Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchaguzi wa Guinea umepongezwa na UM kwa kufanyika kwa amani

Uchaguzi wa Guinea umepongezwa na UM kwa kufanyika kwa amani

Uchaguzi wa kwanza huru kufanyika nchini Guinea tangu nchi hiyo ilipopata uhuru umefanyika jana na kusifiwa na Umoja wa Mataifa.

Hata hivyo waangalizi wameonya kwamba siku zijazo ni muhimu sana na kuwataka viongozi kukubali matokeo yatakayotangazwa. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amepongeza hali ya utulimu na amani wakati wa upigaji kura.

Amesema Waguinea wanasubiri matokeo ya uchaguzi na amezitolea wito pande zote kuendelea kuheshimu wajibu wao katika mchakato wa amani kwa kuzingatia utawala wa sheria na kukubali matokeo. Moja kati ya chama kikuu kilichoshiriki uchaguzi huo leo kimelalamikia ucheleweshaji wa matokeo na kasoro zilizojitokeza katika mchakato wa uchaguzi. Hatua hiyo inatoa ishara ya uwezekano wa mvutano baada ya matokeo.